Nandy afunguka kinachompa pesa tofauti na muziki wa Bongo fleva.anaoufanya

By: Frank Nickson Mapunda
Feb 24 2017
0
  Share on:                 

Msanii muziki wa bongo fleva mwanadada Nandy amebainisha kuwa yeye ni miongoni mwa wasanii nchini Tanzania wanaoingiza kipato cha juu bila ya kutegemea muziki.

Mrembo huyo amesema kuwa amefungua kampuni yake binafsi inayojihusisha na utengenezaji wa nguo za kitenge, mikoba, nguo za harusi pamoja na mavazi mengine ya utamaduni inayojulikana kwa jina la Nandy African Print.

"Nilianza ujasiriamali tokea nipo chuo kabla masuala ya muziki hayajachanganya vizuri nilikuwa naenda kununua nguo Kariakoo halafu ninazipamba vizuri kwa kutumia vitu vya asili". Alisema Nandy

Aidha msanii huyo amesema mpaka sasa ameweza kutoa ajira kwa watu watano ambao ni mafundi wanajishughulisha na utengenezaji wa nguo za asili yaani mafundi cherehani.

"Sijakurupuka kufungua kampuni yangu kwani nilijipanga muda mrefu tokea kipindi ninashiriki mashindano ya muziki nchini 'Nigeria' nikasema nikishinda lazima nitimize lengo langu la muda mrefu, nilianzia na mtaji wa milioni 10 kwa ajili ya kununulia vifaa pamoja na kulipia kodi". Alisema msanii huyo

Kwa upande mwingine msanii huyo alisema malengo ya kampuni yake ni kuhudumia ndani na nje ya nchi kwa kutoa mavazi ya asili yenye ubora zaidi.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako