Gharama ya kuilinda familia ya Trump kwa siku moja itakushangaza!

By: Frank Nickson Mapunda
Mar 20 2017
1
  Share on:                 

Familia ya Rais wa Marekani, Donald Trump ina ulinzi mkali. Ulinzi huo unadaiwa kugharimu kiasi kikubwa cha fedha.

Wakati ambapo Trump alihamia kwenye ikulu ya White House iliyopo jijini Washington DC, mke wake Melanie, na mwanae wa mwisho, Barron bado wanaishi New York.

Muda mfupi baada ya uchaguzi, ripoti ya CNN Money ilionesha kuwa kuilinda familia ya Trump mjini New York hugharimu dola milioni 1 kwa siku.

Kama wakiamua kuungana na Trump White House, gharama hiyo itapungua kwa kiasi kikubwa.

Hilo si jambo pekee linalozungumzwa kwa sasa. Tangu mwaka uanze, Trump ameenda mapumzikoni mara nne huko Mar-a-Lago Florida. Kwa mujibu wa wachambuzi wa gazeti la Politico, safari hiyo hugharimu dola milioni 3 kila akienda.


Maoni
64x64

sucre

Mar 20 2017

Ulinzi unaghalama zake, ndio maana huwezi sikia tajiri kaangukiwa na Dafu.... tutafute pesa.

Acha maoni yako