Kauli ya Irene Uwoya kuhusu mahusiano yake na Mama Watoto wa Aslay.

By: Frank Nickson Mapunda
23 2018
0
  Share on:                 

Msanii wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Irene Uwoya amefunguka kuhusu ukaribu alionao na aliyekuwa mpenzi wa Aslay, Tessy Chocolate.

Siku za hivi karibuni Uwoya ameonekana akiwa karibu sana na Mrembo ambaye amezaa na staa wa Bongo fleva Aslay, Tessy na kujionyesha kama ni mashoga kwa sasa.

Kwenye mahojiano na Bongo 5, Ameongelea ukaribu wake na Tessy, Uwoya amepasua kuwa pamoja na kwamba wanaonekana na ukaribu mkubwa lakini wawili hao wakikutana hawana muda wa kuongelea mabwana kama wengi wanavyofikiri:

Ni mtu ambaye tukikutana tunazungumza mambo ya biashara, lakini ishu zake za mapenzi huwaga sizijui, pia ishu kuhusu mahusiano yake ni privacy, huwa nikikutana naye hatuzungumzi masuala ya mapenzi kwa kwa sababu kila mtu ana wake”.

Sijui kwa sasa yupo na nani kwanza hayanihusu kabisa”.

Tessy baada ya kuachana na Aslay amekuwa akisemekana kuwa Kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na mfanyabiashara maarufu Kwenye mitandao ya kijamii kama Jembe ni Jembe, taarifa ambazo mwenyewe hajazithibitisha.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako