Mwalimu atuhumiwa kumuoa mwanafunzi wake.

By: Frank Nickson Mapunda
23 2018
0
  Share on:                 

Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, Benjamin Siperato.

Ofisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema, mkoa wa Mwanza, Benjamin Siperato ameagiza mwalimu mmoja wa Shule ya Sekondari Nyakasungwa kukamatwa na kuwekwa mahabusu baada ya kukaidi agizo la kumsalimisha ofisini kwake mwanafunzi anayedaiwa kumuoa.

Mwalimu huyo anatuhumiwa kumuoa aliyekuwa mwanafunzi wake mwaka jana ambaye alihitimu mwaka 2016 na kupata daraja la tatu la alama 25, hivyo kuchaguliwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano shule moja iliyoko mkoani Tanga.

Siperato alisema ofisi yake inaendelea kufuatilia kwa makini suala hilo huku akionya kuwa hatua zaidi zitachukuliwa dhidi ya mwalimu yeyote atakayekiuka maadili.

Mwalimu huyo alibainika kumuoa mwanafunzi baada ya baadhi ya wanakijiji wa Nyakasungwa kulalamika kuwa kilichofanyika ni kinyume cha maadili ya kazi yake.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako