Bob Wine kufikishwa mahakama ya kijeshi leo.

By: Frank Nickson Mapunda
23 2018
0
  Share on:                 

Mbunge Robert Kyagulanyi maarufu kwa jina Bob Wine leo anatarajiwa kurudishwa katika mahakama ya kijeshi mjini Gulu kaskazini mwa Uganda.

Taarifa hiyo imewashtua mawakili wake ambao awali walijuzwa kuwa kesi itasikilizwa katika kambi ya kijeshi ya Makindye anakozuiliwa mjini Kampala.

Wakati huo huo Mtandao wa haki za binadamu za wanahabari nchini Uganda umetoa saa 48 kwa jeshi kuwatambulisha askari wake waliowajumu wanahabari.

Kwa upande mwingine, Wanamuziki wakubwa wakiwemo Chris Martin , Angelique Kidjo na Damon Albarn, wametoa wito wa kuachiwa kwa Mbunge Bobi wine ambaye ana wiki sasa tangu kukamatwa kwake na mbunge mwezake na zaid ya watu 30. Wasanii hao wamejaza waraka wa kutaka mbunge huyo wa upinzani kuachiwa.

Wakili wa Bobi Wine anasema kuwa mteja wake ameteswa sana na jeshi, lakini jeshi kwa upande wao wamekanusha.

Bob Wine anatarijiwa kufikishwa mahakamani kwa madai ya kumiliki silaha kinyume na sheria pamoja na tuhuma za wafuasi wake kuushambulia msafara wa Rais Museven.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako