Rais Magufuli amkaribisha Museveni Ikulu.

By: Frank Nickson Mapunda
09 2018
0
  Share on:                 

Rais wa Jamhuri ya Uganda, Yoweri Kaguta Museveni anafanya ziara ya kikazi ya siku moja hapa nchini leo tarehe 09 Agosti 2018. Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano na ujirani mwema uliopo kati ya Tanzania na Uganda.

Mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Museveni amepokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt. John Magufuli. Akiwa nchini, Museveni atakutana kwa mazungumzo ya faragha na Rais Magufuli yatakayofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

Mazungumzo hayo yatafuatiwa na Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Mheshimiwa Rais Magufuli kwa heshima ya Rais Museveni na baadaye leo ataondoka nchini na Ujumbe wake kurejea Uganda.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako