Trumpa azipiga marufuku nguo kutoka Rwanda kuingia Marekani

By: Frank Nickson Mapunda
01 2018
0
  Share on:                 

Rais Donald Trump ametoa agizo hilo akipiga marufuku uondoaji wa ushuru kwa nguo zote zinazotoka Rwanda kwa miezi sita baada ya kukutana na rais Paul Kagame na kumuita rafiki yake.

Kulingana na agizo hilo jipya ni wazi kwamba nguo za Rwanda hazitaingia tena katika soko la nchi hiyo bila kutozwa ushuru.

Serikali ya Marekani inasema kuwa Rwanda imeshindwa kuafikia masharti ya sheria ya AGOA iliopitishwa miaka 18 iliopita kuruhusu bidhaa zaidi za Afrika kuingia nchini Marekani.

Rwanda iliuza nguo zenye thamani ya dola milioni 1.5 nchini Marekani mwaka 2017 lakini hiyo ni asilimia 3 pekee ya bidha inazouza nchini Marekani.

Mwaka 2016, ,majirani wa Afrika mashariki Kenya, Tanzania na Rwanda zilikubaliana kupiga marufuku nguo zilizotumika pamoja na viatu kufikia 2019 ili kulinda viwanda vya nchini .

Kenya na Tanzania zilisalimu amri baada ya Marekani kutishia kupiga marufuku bidhaa zao zinazoelekea nchini humo lakini Rwanda imeendelea kuwekea ushuru mkubwa nguo hizo pamoja na viatu.

Rais Trump na mwenzake wa Rwanda Paul Kagame walijadili biashara walipokutana mnamo mwezi Januari nchini Switzerland lakini hakuna hata mmoja wao aliyezungumzia mzozo kuhusu nguo hizo.

Marekani inadai kwamba marufuku dhidi ya nguo zilizotumika barani Afrika itawanyima raia 40,000 kazi , lakini Rwanda imesema kwamba haitakubali kuwa 'jaa'.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako