Waziri Lugola atoa siku 10 kwa Kaimu Mkurugenzi wa NIDA.

By: Frank Nickson Mapunda
Jul 17 2018
0
  Share on:                 

Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Kangi Lugola ametoa siku zisizozidi kumi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya vitambulisho NIDA, akiwa na kampuni ya Iris Dilham kufika ofisini kwake mjini Dodoma ili kueleza sababu ya kutofika kwa mtambo wa kuchapisha vitambulisho mpaka sasa.

Agizo la Mh. Lugola linakuwa ni utekelezaji wa miongozo aliyopatiwa na Rais Magufuli siku alipomuapisha kuwa Waziri wa Mambo ya ndani baada ya kutengua uteuzi wa Dkt. Mwigulu Nchemba.

Lugola amesema hayo baada ya kutembelea Ofisi ya Uzalishaji vitambulisho hivyo kilichopo Kibaha, mkoani Pwani na kutoridhishwa na kazi ya utoaji wa vitambulisho kwa wananchi, zoezi ambalo linaendelea kufanywa na NIDA katika maeneo mbalimbali nchini.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako