kama kawaida ronardo kupata watoto wengine wawili mapacha huku mama kijacho wa watoto hao bado hajajulikana ni nani

By: Emanuel John
Mar 13 2017
0
  Share on:                 

Kweli Ronaldo ni player tena player haswaa.Wakati dunia nzima kwa sasa inajua kwamba Ronaldo ametulia na kimwana Georginia Rodriguez lakini kumeibuka jipya.Ronaldo ana mwanamke mwenye mimba yake yuko nchini Marekani na anatarajia kuzaa mapacha hivi karibuni.
Taarifa kutoka karibu ya familia ya kina Ronaldo zinasema Ronaldo anatarajia kupata watoto wakiume wawili(mapacha).Inasemekana Ronaldo anajiandaa kumuweka mwanamke huyo katika jengo lake moja lililoko nchini Hispania lenye thamani ya £5m ili kumfanya mwanamke huyo ajifungue sehemu salama zaidi.
Hii sio mara ya kwanza ambapo Ronaldo anazaa na mwanamke asiyejulikana.Mtoto wake kipenzi CR Junior hadi leo haijulikani mama yake yuko wapi.Wakati waandishi wa habari za michezo na wadaku wakihangaika kumtafuta mama mtoto wa Cr7 anaibuka huyu mwingine ambae naye watu wote wameanza kuhangaika kulitafuta jina lake.
Familia nzima ya Ronaldo inajua kuhusu hili na ripoti zinasema wameshaanza kujiandaa kuhamia Hispania ili kwenda kuwasubiria mapacha wao.Ronaldo anaamini ni wakati sahihi sasa kwa mtoto wake wa kiume kuwa na kaka yake lakini bahati imekuja kwa kuwa wanakuja wadogo zake wawili.
Ripoti zingine zinadai mama wa mapacha hao ni Gergina mpenzi wa sasa wa Ronaldo.Lakini Georgina yuko busy na Instagram na picha anazopost zinaonesha kabisa hana mimba.Miezi michache iliyopita Georgina alionekana hadharani na Cristiano Ronaldo lakini hakuwa na dalili yoyote ya mimba.
Dolores ambaye ni mama mzazi wa Cr 7 tayari yuko nyumbani kwa Ronaldo ili kuaanda ugeni wa mapacha hao katika familia yao.Haijatajwa rasmi ni lini haswa mapacha hawa watazaliwa ila inasemekana ni karibuni sana.Swali limekuwa ni nani mama wa mapacha hao?tusubiri muda ufike.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako