Ubora wa zao la korosho kuendelea kuzingatiwa nchini.

By: Frank Nickson Mapunda
May 25 2018
0
  Share on:                 

Serikali kuendelea kuhakikisha kuwa Korosho zinazozalishwa hapa nchini zinakuwa na ubora unaotakiwa katika Soko la Kimataifa ili kuendelea kukuza uzalishaji na kuchochea maendeleo hapa nchini.

Akijibu swali la Mbunge wa Mtwara Vijijini,Hawa Ghasia, Naibu Waziri wa Kilimo,Dkt. Mary Mwanjwelwa amesema kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha kuwa soko la korosho ghafi linaendelea kukua ambapo katika mwaka wa fedha 2017/2018 ilikuwa zuri hususan kutokana na kupanda kwa bei ya korosho na kuuza kuanzia shilingi 3,500 hadi 4,000 kwa kilo.

“Bei ya Korosho ilipanda kutokana na Serikali kuimarisha minada ya Korosho na kuwahamasisha wanunuzi kutoka Vietnam kuja kununua korosho moja kwa moja hapa nchini badala ya kupata korosho hizo kupitia India kama ilivyokuwa imezoeleka kwa muda mrefu” Alisisitiza Dkt. Mwanjelwa

Akifafanua, Mwanjelwa amesema kuwa Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwafanyia uchunguzi wa kina wale wote walioripotiwa katika taarifa Timu ya uchunguzi iliyoundwa na Serikali ili kuhakikisha kuwa wale waliosababisha korosho makontena mawili yaliyogundulika kuwa yalichanganywa na kokoto huko vietnam ambapo ilibainika kuwa korosho hizo zimetoka Tanzania.

Aliongeza kuwa Serikali itachukua hatua mbalimbali ikiwemo kuitaka Bodi ya Korosho Tanzania, Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za ghalani, Tume ya Maendeleo ya Ushirika na Mamlaka za Serikali za Mitaa kushirikiana katika kuimarisha usimamizi wa ubora wa Korosho katika mnyororo wake wote kudhibiti uhalifu huo.

Aidha Mwanjelwa amezitaka Kampuni za ndani na nje ya nchi kuwasilisha malalamiko ya yao Serikalini pale wanapoona mapungufu katika Biashara hiyo badala ya kuzisambaza kwenye mitandao ya kijamii na kwenye vyombo vya habari kwa kuwa kuchafua jina na biashara ya korosho za Tanzania.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako