Kuongezeka kwa kesi za malaria duniani na hofu inavyozidi kutanda

By: Frank Nickson Mapunda
Apr 18 2018
0
  Share on:                 

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 10, inaripotiwa kuwa kesi za malaria duniani hazipungui, jambo ambalo limesababisha wasiwasi jinsi gani bora ifanywe kuukabili ugonjwa huo.

Wataalamu mbalimbali na tajiri mkubwa duniani Bill Gates, wanawahimiza viongozi wa nchi mbalimbali duniani kukusanyika katika mkutano wa kilele wa Jumuiya ya Madola huko London ili kuchanga pesa zaidi kwaajili ya kupambana na ugonjwa huo.

Mwaka 2016, karibu nusu ya watu wote duniani walikuwa katika hatari ya kuambukizwa malaria. kulikuwa na kesi Milioni 216 za malaria katika nchi 91, ongezeko la Milioni tano ikilinganishwa na 2015.

Wataalamu wameeleza kuwa bila uwekezaji zaidi na hatua za kuzuia, litashuhudiwa ongezeko la vifo vinavyotokana na malaria duniani.


Maoni
Currently there are no comments for this topic!
Acha maoni yako