Raia wa Kenya kujipima wenyewe Virusi vya Ukimwi.

By: Frank Nickson Mapunda
May 06 2017
1
  Share on:                 

Kenya imezindua kifaa cha bei nafuu cha kujipimia virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi, ambacho raia wataweza kukitumia bila usaidizi wa daktari.

Ili kujipima, mtu anatoa mate, damu au majimaji kutoka mwilini na kisha anajipima binafsi bila ya kusaidiwa na mtu.

Kifaa hicho kinalenga watu 400,000 ambao hawajafahamu iwapo wana Virusi Vinavyosababisha Ukimwi au la.

Wataalamu wanasema kwamba, kifaa hicho kinafanikiwa asilimia 80, na kitagharimu kama dola 7 hivi na kitapatikana katika maduka ya kuuzia madawa.

Martin Sirengo, kiongozi mkuu wa shirika la kukabiliana na Ukimwi Kenya, Nascop, anasema kuwa bado watu watahitajika kwenda hadi katika vituo vya matibabu ili kuthibitisha matokeo.

Aidha anashauri kuwa, mtu anafaa kujipimia katika sehemu za faragha na mbele ya mtu anayeaminika.

Rudolf Eggers, mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) nchini Kenya, anasema kwamba, “lengo kuu la kifaa hicho cha kujipimia virusi vya HIV ni sambamba na njia nyingine zilizopo za kupima HIV.”

Takriban watu milioni 1.5 wanaishi na virusi vya HIV nchini Kenya, ambapo milioni moja kati yao wanatumia matibabu ya kumeza vidonge vya kupunguza makali ya ugonjwa wa Ukimwi.


Maoni
64x64

anyah

Feb 04 2018

Am Anyah kutoka Singapore. Ninataka kupitisha hili kwa kila mtu ambaye ni mgonjwa wa aina yoyote ya ugonjwa, suluhisho la magonjwa yote ni Dr Sagbo, niliponwa na mtu huyu Mheshimiwa Sagbo mponya mkuu baada ya kupita kwa maumivu. Sijui kamwe nitaponywa ugonjwa huu wa Hiv katika maisha yangu kwa sababu walisema hakuna tiba. Ninajaa msisimko na nina kutumia hii kati ili kukujulisha kuwasiliana na mtu huyu kwa aina yoyote ya ugonjwa na yuko tayari kusaidia kutatua tatizo lako. Ikiwa unapitia magonjwa yoyote kwa njia ya kumsiliana naye kwa njia ya barua pepe yake: drsagbo6088@gmail.com. Ninaweka ahadi yangu kwa kugawana ushuhuda huu ninawahakikishia wale wote ambao walisema kuwa hakuna tiba mbaya ya sababu nimekuwa tubiwa na dawa za dawa za Dr Sagbo mponyaji mkuu, lengo langu ni kushika ushuhuda juu ya kile ambacho Mungu ametumia wewe kufanya katika maisha yangu. Piga simu na nambari hii na whatsapp yake kwenye +2347019642881.

Acha maoni yako